
Maporomoko ya ardhi yameua watu wasiopungua wanane na kusababisha zaidi ya 80 wakiwa hawajulikani walipo leo Jumamosi, Januari 24, huko Java, kisiwa kikuu cha Indonesia, shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga limeripoti.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Java, kisiwa kikuu cha nchi hiyo inayopakana na bara, kilikumbwa na maporomoko ya ardhi mapema Jumamosi. Shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga limeripoti watu 83 kutoweka.
“Maporomoko ya ardhi yalitokea katika eneo la West Bandung la mkoa wa West Java mapema Jumamosi, na kuua watu wanane,” amesema Abdul Muhari, msemaji wa shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga, akiongeza kuwa watu 83 hawajulikani walipo.
Majanga ya mara kwa mara
Majanga haya hutokea mara kwa mara nchini Indonesia wakati wa msimu wa mvua, ambao kwa kawaida huanza mwezi Oktoba hadi mwezi Machi na husoma ardhi. Wataalamu wa mazingira wanataja ukataji miti kama moja ya sababu, kwani misitu husaidia kunyonya mvua na kuimarisha udongo kutokana na mizizi ya miti. Kupotea kwa maeneo yenye misitu hufanya maeneo haya kuwa hatarini zaidi kwa mafuriko ya ghafla na maporomoko ya ardhi.
Mapema mwezi huu, watu 16 walifariki katika kisiwa cha Siau cha Indonesia, huko Sulawesi, na mafuriko ya ghafla kufuatia mvua kubwa. Mnamo mwezi Novemba, majimbo matatu katika kisiwa cha magharibi cha Sumatra yaliharibiwa na mafuriko yaliyowaua watu wapatao 1,200 na kusababisha wengine 240,000 kuyahama makazi yao, kulingana na shirika la kitaifa la usimamizi wa maafa.
Mapema wiki hii, serikali ya Indonesia ilitangaza kufuta vibali kwa makampuni 28, ikiwa ni pamoja na makampuni 22 ya ukataji miti, kampuni moja ya madini, na shirika moja la ujenzi wa mitambo ya umeme wa maji. Uchimbaji madini, mashamba makubwa, na moto vimesababisha kutoweka kwa maeneo makubwa ya msitu wa mvua wenye rutuba wa Indonesia katika miongo ya hivi karibuni, kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali.