Chanzo cha picha, Getty/Reuters
Mjumbe wa Marekani Steve Witkoff na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Iran Abbas Araqchi wameelekea Uswisi kwa mazungumzo, shirika la Axios
liliripoti siku ya Ijumaa, huku usitishaji wa mapigano nchini Lebanon
ukionekana kufufua juhudi za kubadilisha makubaliano ya muda ya kusitisha vita
vya Iran kuwa mpango wa kudumu wa kikanda.
Israel na Hezbollah walikubaliana kusitisha mapigano nchini
Lebanon siku ya Ijumaa baada ya kuongezeka kwa mapigano yaliyotia shaka
mazungumzo kati ya Marekani na Iran, ambayo ni muhimu kwa ajili ya kufunguliwa
tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz na kuleta utulivu wa usambazaji wa mafuta.
Hatua hiyo ilifuatia hati ya makubaliano yenye vipengele 14
ambayo pande hizo mbili zilitia saini wiki hii ili kusitisha mapigano na
kufungua kipindi cha siku 60 cha kutatua mizozo kuhusu mpango wa nyuklia wa
Iran, pamoja na masuala mengine magumu yanayohitajika ili kufikia makubaliano
ya kudumu zaidi.
Hata hivyo, makamu
wa Rais wa Marekani JD Vance aliahirisha mipango siku ya Alhamisi ya kusafiri
hadi Uswizi kwa mazungumzo hayo, huku kukiwa na mvutano unaoongezeka nchini
Lebanon kati ya Israel na Hezbollah, kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na
Iran.
Huku usitishaji
mapigano ukiwa umeanza kutekelezwa, Witkoff anaelekea Uswizi kuungana na Jared
Kushner, mkwe wa Rais Donald Trump, ambaye tayari yuko huko, Axios alisema.
Araqchi anapanga kusafiri leo Jumamosi, iliongeza.
Soma zaidi: