Serikali ya Kongo imetangaza Januari 27, 2026, “siku ya kuwakumbuka waathiriwa wa ukatili uliofanywa na muungano wa jeshi la Rwanda na M23-AFC katika miji ya Bunagana na Uvira,” mashariki mwa nchi. Maadhimisho haya yamefanyika mwaka mmoja baada ya jiji la Goma kuangukika mikononi mwa kundi lenye silaha, linaloungwa mkono na Rwanda. Sherehe ilifanyika katika Chuo cha Sanaa huko Kinshasa, mbele ya Waziri Mkuu. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Paulina Zidi

Wimbo wa taifa ulipigwa katika Chuo cha Sanaa kuadhimisha siku hii, ambayo serikali ilikusudia kuwa ya kiishara. “Ni kwa hisia kubwa ninapozungumza katika siku hii ya kumbukumbu, si ya kukumbuka maumivu ya wale walio miongoni mwa watu wetu ambao walipoteza maisha,” Waziri Mkuu Judith Suminwa alitangaza. “Inatukumbusha maisha yaliyokatizwa, familia zilizo na majeraha milele, na taifa linalokabiliwa na mateso makali zaidi katika historia yake ya hivi karibuni.”

“Ikiwa mumechagua kuadhimisha siku hii ya kumbukumbu, ni kwa sababu kumbukumbu ni kitendo cha uwajibikaji. Kumbukumbu inatulazimisha, inatutia nguvu. Siku hii inatukumbusha kwamba kinachotokea leo katika sehemu ya mashariki ya nchi yetu kinahusu taifa zima, uadilifu wake wa eneo, heshima yake, na mustakabali wake,” aliongeza Patrick Muyaya, Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali.

“Tunataka amani”

Maadhilisho ya kumbukumbu ambayo Olivier, mwandishi wa habari kutoka Goma, aliyehamia Kinshasa mwaka mmoja sasa, hakutaka kukosa. “Hili ni muhimu sana kwa sababu ulimwengu mzima unahitaji kujua kinachoendelea DRC na kilichotokea Goma. Kumekuwa na mauaji; hawa ni waasi. Walifika na kuwatishia watu. Na leo, watu wametawanyika. Mimi mwenyewe niko hapa, lakini familia yangu haipo pamoja nami.”

Na katika chumba hicho, wakazi kadhaa wa Kinshasa walikuja kuonyesha uungwaji wao mkono: “Mamilioni ya vifo hayawezi kusahaulika. Lazima tukumbuke hili na tusimame kwa muda kufikiria kuhusu mamilioni ya Wakongo ambao wamepoteza maisha mashariki mwa nchi yetu,” alisema mshiriki mmoja. “Ujumbe pekee ninaotaka kuwasilisha ni kwamba tunataka amani,” mwingine aliongeza. “Tumeteseka sana. Na ni leo ambapo hatimaye, pamoja na raia wa Kongo hapa, tunaweza kusema hapana kwa uchokozi wa Rwanda.” 

Mwishowe, mishumaa iliwashwa kama heshima kwa waathiriwa wa vita hivi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *