#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) kuwaweka ndani Mkandarasi na Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Nguzo Nane hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa kupuuza maagizo ya Mkuu wa Mkoa Mboni Mhita.
Waliowekwa ndani ni Mkandarasi Edwin Rwezahula na Mhandisi Mshauri Emmanuel Kisimba.
Agizo hilo amelitoa jana wakati alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa yaliyotolewa Januari 5, mwaka huu, juu ya kuendelea kwa ujenzi wa barabara hiyo, na kubaini hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika tangu RC Mhita alipotoa maagizo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania