#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limetoa msaada wa shilingi 816,000 kwa familia ya mtoto Imani Chakupewa ili kumwezesha kuanza masomo ya kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Manyara Boys.

Hatua hii imekuja baada ya vyombo vya habari hususan ITV kuripoti changamoto ya mtoto huyo mkazi wa Kijiji cha Mduwi, ambaye alikuwa ameshindwa kuripoti shuleni kutokana na wazazi wake kukosa uwezo wa kumudu gharama za nauli, sare, na vifaa vya shule.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Issa Suleiman, ameeleza kuwa jeshi hilo limeguswa na taarifa hiyo na kuamua kuchukua hatua kama sehemu ya ushirikiano wao na jamii.

Kamanda Suleiman amesisitiza kuwa kumsaidia mtoto huyo kupata elimu ni njia mojawapo ya kuzuia uhalifu, kwani kukaa mtaani bila shughuli maalumu kunaweza kumfanya ajiingize katika vitendo viovu, hivyo jeshi limeona ni vyema kuwekeza katika mustakabali wake wa kielimu.

Kwa upande wake, familia ya Imani imelishukuru Jeshi la Polisi na vyombo vya habari kwa kuibua na kutatua changamoto hiyo, wakikiri kuwa walishakata tamaa ya kumsomesha mtoto wao kutokana na hali duni ya kiuchumi.

Kamanda Suleiman amevipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya kuibua kero za kijamii na kutoa rai kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya msingi ya elimu.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *