#HABARI: Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka kipaumbele katika utunzaji wa mazingira, ikiwemo utamaduni wa kupanda miti kila tarehe 27 Januari kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa rasilimali za asili zinalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kile kijacho.

Wizara ya Katiba na Sheria imeunga mkono maono hayo kwa vitendo kupitia zoezi la upandaji miti lililofanyika Mtumba, Dodoma. Zoezi hilo liliongozwa na Naibu Waziri Mhe. Zainab Katimba pamoja na Katibu Mkuu Eliakim Maswi, likihusisha menejimenti na watumishi wa wizara ili kuonyesha mchango wa sekta ya sheria katika kutatua changamoto za mazingira.

Uhifadhi wa mazingira ni suala mtambuka linalohitaji ushirikiano kati ya watumishi wa umma na jamii nzima. Kwa kuwa mazingira salama ni msingi wa haki za binadamu, jitihada hizi ni muhimu katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali na kuhakikisha ustawi wa taifa kwa ujumla.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *