
Siku ya Alhamisi, Januari 29, siku moja baada ya shambulio la uwanja wa ndege wa Niamey na watu wenye silaha, maisha yamererejea katika hali ya kawaida katika mji mkuu.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais Abdourahamane Tiani alizuru kambi ya wanajeshi, sehemu ya uwanja wa ndege inayohifadhi vyombi vya anga vya jeshi. Alisifu ushujaa wa wanajeshi wa Niger na Urusi waliowarudiha nyuma washambuliaji na kuwatuhumu marais wa Ufaransa, Benin, na Côte d’Ivoire. Tiani alisema kwamba marais hao waliwaunga mkono mamluki waliohusika na shambulio hilo.
Maelezo zaidi yameibuka kuhusu shambulio hili kubwa katika kambi ya 101 jeshi la anga, ambalo lilitokea usiku wa Jumatano, Januari 28, kuamkia Alhamisi, Januari 29. Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi, washambuliaji 20, walioelezewa kama “mamluki,” waliangamizwa na 11 walikamatwa. Ripoti ya televisheni ya serikali RTN inadai kwamba raia wa Ufaransa alikuwa miongoni mwa washambuliaji waliouawa, bila kutoa maelezo zaidi. Wanajeshi wanne wa Niger walijeruhiwa vibaya.
Alipozuru kambi ya 101 ya jeshi la anga siku ya Alhamisi, kiongozi wa utawala wa kijeshi, Jenerali Abdourahamane Tiani, aliwasifu wanajeshi na washirika wao wa Urusi ambao, kutokana na “mwitikio wao wa haraka,” waliweza, kulingana naye, “kumshinda adui ndani ya dakika 20” baada ya risasi za kwanza kufyatuliwa.
Macron, Talon, na Ouattara, “wadhamini wa mamluki”
Akizungumza kwa hasira, Rais Tiani kisha aliwashambulia wale aliowaita “wadhamini wa mamluki hawa”: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Rais wa Benin Patrice Talon, na Rais wa Côte d’Ivoire Alassane Ouattara. “Tumewasikiliza wakibweka vya kutosha. Waache, nao, wajiandae kutusikiliza tukinguruma,” alionya. Abdourahamane Tiani hakufafanua vitisho hivi.
Tunawakumbusha wadhamini wa mamluki hawa kwamba tumewasikiliza wakibweka vya kutosha; waache, nao, wajiandae kutusikiliza tukinguruma.
Siku ya Alhamisi, mikutano miwili mikubwa ilifanyika siku nzima, mmoja mbele ya Bunge la taifa na mwingine katika makutano makuu karibu na kambi ya jeshi la anga.
Kulingana na Wizara ya Ulinzi, uharibifu mkubwa wa vifaa kwa ndege ulisababishwa wakati wa shambulio hilo, haswa kwa ndege mbili za shirika la ndege la Asky na moja kwa Air Côte d’Ivoire. Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu uharibifu wa sehemu ya kijeshi ya uwanja wa ndege. Shirika la Kitaifa la Usafiri wa Anga, kwa upande wake, lilionyesha kuwa shughuli za uwanja wa ndege “zinaendelea kawaida.”