Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mtandaoni kuhusu benki hiyo kuwa na mpango wa kuuza hifadhi ya dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.3 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati, ambayo imepunguziwa ufadhili na taasisi za kimataifa.

Emmanuel Akaro ni Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, amezungumza na wanahabari kuhusiana na uvumi huo ambapo amesema madai hayo si ya kweli, ila kilichopo ni mpango wa kuuza hifadhi ya dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa ili kuweka sawa mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki kuu.

Amesema Bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi thamani ya dola bilioni 2, huku thamani ya sasa ya hifadhi hiyo ikiwa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo benki inapanga kuuza kiasi cha dhahabu kilichozidi.

#kilichoborakabisa

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *