Katika taarifa iliyotolewa leo Januari 30, 2026 huko Geneva, Mkuu wa Mawasiliano wa UNICEF nchini Sudan, Eva Hinds, amesimulia yale aliyoshuhudia na ugumu wa kuwafikia watoto katika eneo la Darfur akisema Sudan ndio janga kubwa zaidi la watoto ulimwengu. 

“Ndani ya Darfur leo, kumfikia mtoto mmoja tu kunaweza kuchukua siku kadhaa za mazungumzo, vibali vya usalama, na kusafiri kwenye barabara za vumbi katika hali yenye matukio yasiyotabirika kila wakati.” 

Hinds ameeleza kuwa kila hatua ya msaada ni ya kufa na kupona na kila uwasilishaji wa misaada umekuwa dhaifu kutokana na mapigano yanayoendelea.

Mtoto mdogo amesimama mbele ya hema la muda katika kambi ya wakimbizi wa jangwa huko Tawila, Darfur Kaskazini, Sudan, baada ya kufukuzwa kwa sababu ya migogoro inayoendelea. UNICEF na washirika wake wanatoa msaada wa dharura.

© UNICEF/Mohammed Jamal

Mtoto amesimama mbele ya hema katika makazi ya muda katika kambi ya wakimbizi huko Tawila, Darfur Kaskazini, kufuatia kuhama kutokana na vita vinavyoendelea.

Licha ya hali hiyo, UNICEF na washirika wake wamefanikiwa kutoa chanjo kwa watoto zaidi ya 140,000 ndani ya wiki mbili pekee, huku maelfu wakipatiwa matibabu ya utapiamlo na magonjwa mengine. Eva Hinds amesisitiza umuhimu wa msaada huo.

 “Ni kazi inayofanyika kwa uangalifu na hatari kubwa, inayofikishwa kwa kutuma msafara mmoja unaosaidia kliniki moja, na darasa moja kwa kila safari, na hii ndio maana kuwa watoto wa Darfur, wapo kwenye hatihati ya kati ya kutelekezwa na kufikiwa.”

Amesema kuwa kile alichokishuhudia huko katika safari yake ya siku kumi hawezi kukifananisha na jambo lolote alilowahi kuliona maishani mwake katika maeneo yenye dharura. Akisimuliza visa vya watoto walioachwa yatima huku wakikabiliwa na utapiamlo lakini bado wana matumaini ya kurudi shule.

Tawila ni mji ulioteketea

Hinds amesema ameshuhudia hali ya kushtua huko Tawila, ambapo mji mzima umejengwa upya kutokana na machafuko Kusimama ndani ya eneo lile kubwa la makazi duni, nyasi, miti, na plastiki ilinilemea. Inaonekana kama mji mzima uling’olewa na kujengwa upya kwa sababu ya kuhitaji malazi na hofu.” 

UNICEF imetoa wito wa hatua madhubuti ili kuzuia athari mbaya kwa watoto wa Sudan ambao wapo ukingoni kuangamia kwa matumaini kuwa ulimwengu utasikia vilio vya watoto hawa na kutoa msaada zaidi wa chakula,vifaa vya malazi, na huduma za afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *