
Wakati wa hafla ya kuweka msingi wa mradi huo hapo jana, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Christopher Landau, alisema lazima wawaonyeshe wale wanaopanga kushambulia kwamba wamedhamiria kujilinda.
”Kambi hii inaonyesha dhamira inayoonekana wazi, ulinzi wa pamoja kati ya Marekani na Kenya. Inatoa ishara kali kwa wale wanaopanga kuwa maadui zetu.”
Kambi hiyo ya Manda Bay hutumiwa na vikosi vya Marekani na kwa muda mrefu imekuwa kitovu cha kimkakati katika vita dhidi ya kundila Al-Shabaab lenye mafungamano na Al-Qaeda.