“Mwakilishi mwandamizi wa kidiplomasia wa Afrika Kusini, … Shaun Edward Byneveldt, hatakiwi kuwepo hapa nchini na lazima aondoke Israel ndani ya saa 72,” wizara ilisema kupitia taarifa, ikiongeza kuwa “hatua zaidi zitachukuliwa katika kipindi kifaacho.”

Balozi wa Israel kufukuzwa

Mapema siku ya Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini ilitangaza kuwa kaimu balozi wa Israel nchini Afrika Kusini, Ariel Seidman, amefukuzwa nchini humo kutokana “na mfululizo wa ukiukwaji wa taratibu za kidiplomasia ambazo ni changamoto kwa uhuru wa Afrika Kusini,” ikiwemo kile kinachoonekana kama kumtukana Rais Cyril Ramaphosa.

Afrika Kusini pia ilimtaka Seidman kuondoka nchini katika kipindi cha saa 72.

Seidman amekuwa balozi mdogo wa Israel tangu Novemba 2023, wakati Israel ilipomrejesha nyumbani balozi wao nyumbani baada ya Afrika Kusini kuwaondoa wanadiplomasia wao nchini Israel kutokana na vita vya mauaji ya halaiki vya nchi hiyo huko Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *