DAR ES SALAAM: Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-CENTRE), David Kafulil amesema ziara ya Rais wa Singapore,  Tharman Shanmugaratnam imeleta hamasa kwa serikali, wanazuoni, jumuiya za wawekezaji na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza leo Juni 10, Dar es Salaam amesema hatua hiyo ni kutokana na muujiza wa Singapore ilivyomudu kupaa kutoka nchi ya dunia ya tatu( ya watu masikini) mpaka dunia ya kwanza kwa ubora wa maisha ya watu.

Amesema takwimu za IMF 2026, zinaonesha Singapore ni nchi ya 5 kwa pato la mtu( per capital) iliyofikia Dola 107000.

“Ingawa Singapore sio miongoni mwa mataifa 21 yenye chumi kubwa zaidi duniani( Trilion dollar club- nchi ambazo uchumi wake ni zaidi ya dola trilion1), lakini uchumi wa Singapore mwaka 1995 ulikuwa sawa na Tanzania. Ulikuwa Dola billion 87,” amesema Kafulila.

Amesema, ikiwa leo zaidi ya miaka30, Singapore uchumi wake haujafika dolla Trilion1(umefika dola billion 659), tafsiri yake, inahitajika kasi zaidi ya Singapore kuelekea 2050 ili kufikia uchumi wa Dola trilioni 1.

“Nadhani ndio msingi wa kauli ya Rais wetu, Dk Samia Suluhu Hassan kusema kwamba kufikia Dira2050 tunahitaji sio tu kubadilika bali kubadilika jinsi na namna tunavyofanya kwa kiasi kikubwa,” ameongeza.

Rais Tharman Shanmugaratnam alisisitiza umuhimu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi( PPP) na kuhitimisha kwa kutaka Serikali za Afrika ziache kufanya miradi inayoweza kufanywa na Sekta binafsi ili kuongeza ufanisi na zaidi kuelekeza rasilimali kidogo ilizonazo kwenye eneo la ujenzi wa rasilimali watu yenye ubora kwani rasilimali watu ndio sarafu ya dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *