Dar es Salaam. Simba imetangaza nafasi mbili za ajila ndani ya Klabu hiyo huku mojawapo ikiwa ni ya Mkurugenzi wa Ufundi ambayo ni kwa mara ya kwanza imeanza kuwepo ndani ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba leo Jumamosi, Januari 31, 2026, Mkurugenzi huyo wa ufundi wa Simba atakuwa na majukumu ya kufuatilia mipango ya muda mrefu, ksuimamia usajili na uhamisho, kufanya tathmini ya benchi la ufundi na kusimamia.

Hii ni mara ya kwanza kwa Simba kuwa na mkurugenzi wa ufundi, nafasi ambayo ni daraja baina ya uongozi wa timu na benchi lanufundi.

Taarifa ya Simba imeeleza kwamba muombaji anapaswa kuwa na leseni ya ukocha ya daraja A CAF na kinyume cha hapo basi ni awe na leseni daraja A ya Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA).

Sifa nyingine ni awe na shahada ya kwanza au stashahada ya Sayansi ya Michezo au utawala na pia awe na ufahamu wa mifumo ya kisoka.

Mbali na nafasi hiyo, Simba pia imetangaza nafasi ya Mkurugenzi wa Wanachama ambayo katika miaka ya hivi karibuni ilikuwa inashikiliwa na Mzee Hamisi Kisiwa).

Kwa mujibu wa taarifa ya Simba, Mkurugenzi huyo wa Wanachama wa Simba anapaswa awe angalau ana uzoefu wa miaka mitatu wa nafasi hiyo au inayofanana nayo na awe na shahada ya kwanza masoko, utawala wa kibiashara.

Taarifa ya Simba imeeleza kuwa Mkurugenzi huyo wa wanachama atatakiwa kufanya mambo manne ya msingi ambayo ni usajili wa wanachama, kuwakutanisha pamoja wanachama na kufanya nao mawasiliano, kufanya tathmini ya data na mkakati, kuongeza idadi ya wanachama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *