Dar es Salaam. Wengi wana zaidi ya 40. Lakini wale ambao miaka yao haiongezeki sasa ni rasmi wana miaka 40. Na wengi wao ni washiriki wa Miss Tanzania 2006, msimu huo wa umiss ulizalisha mastaa wengi.

Wema Sepetu, Jokate Mwogelo, Irene Uwoya, Lissa Jensein na Anti Ezekiel. Ni Anti pekee ndo hakuwepo 5 bora. Wote sasa ‘eji’ imesogea sana kwa sasa wakiwa na 40 na ushee.

Ni miaka 20 sasa imepita tangu lifanyike shindano hilo. Na kwa kawaida washiriki ni wa miaka zaidi 18. Baada ya kumaliza shule na walizuga kitaa ndo wakashiriki umiss. Bila shaka.

Kwa vyovyote iwavyo wengi wao wana miaka 40 sasa. Hata kama kuna mwenye upungufu basi ni miaka 38 hadi 39. Kwa hiyo mtu kama Wema atakuwa na 38 au 39 keshi bila chenji. 

Wafanye ‘besidei’ zao bila kuweka umri, ila ‘wahuni’ wajue wale siyo Gen Z ni mishangazi. Kilometa zimekata za kutosha sana mpaka sasa. Miaka inaenda kasi sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *