Akizungumza na kituo cha CNN siku ya Jumapili (Februari 2), Araghchi alisema kwa bahati mbaya, nchi yake imepoteza imani na Marekani kama mshirika wa majadiliano.

Alipoulizwa ni vipi kunaweza kuwapo mchakato wa mazungumzo wenye manufaa, Araghchi alikiambia kituo hicho kwamba lazima pande zote ziishinde hali ya kutoaminiana iliyopo.

Kauli hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Iran imetolewa wakati kukishuhudiwa kiwango fulani cha maendeleo kuelekea majadiliano baina ya Washington na Tehran mwishoni mwa wiki.

Araghchi aliiambia CNN kwamba nchi yake imekuwa ikishirikiana na baadhi ya mataifa rafiki na jirani yamekuwa yakijenga mazingira ya imani na kuanzaa majadiliano ya kina.

Rais Donald Trump wa Marekani aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kwamba Iran ilikuwa inazungumza na Marekani. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *