
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka serikali ya Israel, Mamlaka ya Palestina na Umoja wa Ulaya vimethibitisha kuwa watu wataruhusiwa kuingia na kutoka ingawa kwa idadi ndogo siku ya Jumatatu (Februari 2) wakati majadiliano yakiendelea juu ya hatua za kiusalama na kiuendeshaji.
Kufunguliwa kwa kituo hicho muhimu kwa maisha ya Wapalestina kilichofungwa kwa zaidi ya mwaka sasa ni sehemu ya kile kiitwacho “mpango wa amani wa Rais Trump kwa Gaza”.
Watu wapatao 150 wanatazamiwa kuruhusiwa kuondoka Ukanda huo kila siku kutoka leo, huku wengine 50 wakiruhusiwa kurejea, lakini mamlaka za Israel zimesema ni Wapalestina 42,000 tu waliokimbia Gaza wakati wa vita ndio wataruhusiwa kuingia.
Kwa mujibu wa wizara ya afya kwenye Ukanda huo, kiasi cha wagonjwa 20,000 wanangojea kuingia Misri kwa matibabu, huku 440 kati yao wakiwa na hali mbaya kabisa.
Wagonjwa 4,000 wa saratani na watoto 4,500 wamo pia kwenye orodha ya dharura.