
Chini ya mwaka mmoja baada ya ziara yake ya mwisho, Gérald Darmanin anafanya ziara nyingine rasmi nchini Morocco leo Jumatatu, Februari 2 na kesho Jumanne, Februari 3, ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimahakama kati ya Paris na Rabat, hasa katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Casablanca, Matthias Raynal
Waziri wa Sheria wa Ufaransa Gérald Darmanin ambaye hufanya ziara mara kwa mara nchini Morocco, ambapo ziara yake ya mwisho aliifanya chini ya mwaka mmoja uliopita – mnamo mwezi Machi 2025 – anafanya ziara nyingine rasmi nchini Morocco leo Jumatatu, Februari 2 na kesho Jumanne, Februari 3, akiwa na lengo moja: kuimarisha ushirikiano wa kimahakama kati ya Rabat na Paris, hasa katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na ujambazi uliokithiri.
Ziara ya Gérald Darmanin inakuja wakati ambapo ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umeimarika katika nyanja hii katika miezi ya hivi karibuni. Mnamo mwezi Januari 2025, Morocco ilimrejesha nyumban nchini Ufaransa Félix Bingui, mtu anayeshukiwa kuwa kiongozi wa kundi la Yoda lenye makao yake Marseille.
Miezi mitano baadaye, mwezi Juni, Mohammed Bajjou, Mfaransa mweye asili ya Morocco, anayeshukiwa kupanga visa kadhaa vya utekaji nyara katika ulimwengu wa sarafu za kidijitali, alikamatwa huko Tangier. Ufaransa sasa inataka arudishwe nyumbani.
Ushirikiano mkubwa wa kimahakama kati ya Paris na Rabat
Hatimaye, mwezi Agosti mwaka uliyopita, washirika wawili wanaodaiwa kuwa wa mfanyabiashara wa dawa za kulevya Mohamed Amra—ambaye alitoroka kutoka kwenye gari la gereza nchini Ufaransa mnamo mwezi Mei 2024 na kusababisha vifo vya walinzi wawili wa gereza—walihamishiwa Ufaransa, miezi sita tu baada ya kukamatwa kwao nchini Morocco. Tukio ambalo, Gérald Darmanin alichapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akiwashukuru viongozi wa Morocco, haswa “Waziri mwenzake wa Sheria,” ambaye “alifanya operesheni hii iwezekane haraka sana.”
Wakati wa ziara hii ya hivi karibuni nchini Morocco, Gérald Darmanin anatarajiwa kukutana naye tena, na mkutano na Waziri wa Mambo ya Ndani pia umepangwa.