Polisi wa Hong Kong wamesema watu wanne wameshtakiwa kwa kula njama ya kumwibia mwanamume Mjapani yeni milioni 51, au karibu dola 330,000 za Marekani, pesa taslimu.

Februari mosi, polisi walisema kwamba walioshtakiwa kwa wizi huo wa Januari 30 huko Hong Kong ni Wajapani watatu na Mchina mmoja. Waliongeza kuwa wanne hao ni miongoni mwa watu sita ambao tayari walikuwa wamekamatwa kutokana na tukio hilo.

Wawili kati ya Wajapani hao watatu wanatuhumiwa kutekeleza wizi huo.

Mjapani mwingine anayeshtakiwa anashukiwa kuhamisha pesa taslimu wakiwa na mwanamume huyo aliyeibiwa hadi Hong Kong. Pia inadaiwa alitoa ratiba ya usafiri na taarifa zingine kwa kundi lililohusika na wizi huo.

Polisi wamesema wataendelea na uchunguzi wao kwa watu wengine wawili waliokamatwa, mmoja Mchina na mwingine kutoka Hong Kong, kwa hiari. Polisi wanashuku kwamba wawili hao walisaidia kwenye kubadilishana pesa taslimu zilizoibwa.

Mahakama huko Hong Kong inapanga kusikiliza kesi hiyo kwa mara ya kwanza Februari 2, huku wale walioshtakiwa wakihudhuria. Waendesha mashtaka wanatarajiwa kubainisha mashtaka hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *