Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila imesema imeandaa kambi maalumu ya kutengeneza na kurekebisha mishipa ya kuchuja damu (Arterio-Venous Fistula Creation) ili kuwasaidia wagonjwa wa figo nchini. Kambi hiyo inayotarajiwa kufanyika kwa siku tano inatarajiwa kuanza Februari 14 na kukamilika Februari 18, 2026 katika hospitali hiyo.
Taarifa ya Esterbella Malisa
Mhariri @moseskwindi