Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baqaei amelaani mashambulizi ya kikatili ya Marekani dhidi ya meli za kibiashara za India, na kusisitiza kuwa mashambulizi hayo ya Marekani katika Bahari ya Oman ni uharamia wa serikali.

Baqaei ameandika katika akaunti yake ya X kwamba: Mashambulizi ya kikatili ya Marekani dhidi ya meli za kibiashara ambayo yameua raia wa India wasiopungua watatu ni ushahidi wa wazi wa sera ya Marekani ya ujambazi wa kutumia silaha na uharamia wa serikali.”

“Tunatoa mkono wa pole kwa familia na marafiki wa mabaharia wa India waliouawa, na tunatuma rambirambi zetu za dhati kwa wananchi na serikali ya India,” ameandika Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.

Esmaeil Baqaei amesisitiza kuwa jamii ya kimataifa lazima iiwajibishe Marekani kwa vitendo vyake vilivyo kinyume cha sheria vinavyoendelea kutishia amani na usalama duniani na kuhatarisha uhuru wa usafiri wa majini.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza haya huku hali ya wasiwasi ikiendelea kuongezeka kufuatia mashambulizi mtawalia ya Marekani dhidi ya meli za kibiashara za India katika Bahari ya Oman.

Siku ya Alhamisi, Kamandi Kuu ya Marekani ilisema kuwa ndege ya Marekani ilirusha makombora mawili ya Hellfire kwenye chumba cha injini ya meli ya mafuta ya Jalveer, ikidai kuwa meli hiyo ilikuwa ikisafirisha mafuta ya Iran. Serikali ya India imesema kuwa wafanyakazi wote 20 wa meli hiyo walikuwa salama na walihamishwa kwa msaada wa Oman.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *