#HABARI: Mwanaharakati na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Habibu Mchange, ametoa onyo kali kwa viongozi wa Chadema akituhumu kuwepo kwa ubadhirifu wa michango ya umma na usambazaji wa maudhui ya chuki yenye lengo la kuchafua taswira ya Taifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mchange amedai kuwa viongozi hao wanatumia makala za kimataifa na video za vurugu kubadilisha ajenda za kitaifa na kuvuruga amani ya nchi.
Mchange ametoa mchanganuo wa fedha za michango ya Mwenyekiti Tundu Lissu, akidai kuwa jumla ya shilingi milioni 41 zilipatikana, lakini kiasi kilichotangazwa kwa umma ni shilingi milioni 26 pekee.
Ameongeza kuwa wakati familia ya Lissu ikipokea shilingi milioni 22, kiasi kilichosalia cha shilingi milioni 19 kinadaiwa kuhamishwa kwenda kwa wanaharakati jijini Nairobi, Kenya, kwa maelekezo ya John Heche ili kufadhili harakati dhidi ya Serikali.
Aidha, mchambuzi huyo amewatuhumu viongozi hao kwa kukusanya michango ya rambirambi kufuatia kifo cha muasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei, na kudai kuwa hadi sasa kiasi hicho hakijulikani kilipo.
Mchange amewataka wananchi kuwa makini na michango hiyo huku akisisitiza kuwa vitendo hivyo ni sehemu ya mikakati ya viongozi wa Chadema kujinufaisha na fedha za wafuasi wao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)