• Azimio la Umoja imemteua kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kama kiongozi mpya wa chama chake kufuatia mkutano wa ngazi ya juu wa NEC
  • Rais wa zamani Uhuru Kenyatta aliongoza mkutano huo ambao pia ulishuhudia Mbunge wa Suba Kaskazini, Caroli Omondi akiteuliwa kuwa katibu mkuu
  • Msajili wa Vyama vya Siasa alithibitisha mabadiliko hayo na kumwagiza Azimio kuyachapisha kulingana na Sheria ya Vyama vya Siasa

Chama cha Muungano cha Azimio la Umoja–One Kenya kimetangaza mabadiliko makubwa ya uongozi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Kalonzo Musyoka at Raila's grave
Kalonzo Musyoka alipozuru kaburi la Raila Odinga huko Bondo, Kaunti ya Siaya. Picha: Kalonzo Musyoka.
Source: Facebook

Kalonzo Musyoka wa Wiper Patriotic Front aliteuliwa kuwa kiongozi mpya wa chama hicho cha muungano, katika hatua inayoashiria awamu mpya kwa chama cha upinzani.

Mabadiliko hayo yaliidhinishwa wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Kitaifa ulioongozwa na rais wa zamani Uhuru Kenyatta.

Uongozi mpya wa Azimio La Umoja

Katika kikao hicho hicho, Mbunge wa Suba Kaskazini, Caroli Omondi, aliteuliwa kuwa katibu mkuu, akichukua nafasi ya mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohammed, ambaye alikuwa ameshikilia nafasi hiyo yenye ushawishi tangu kuundwa kwa muungano huo.

Pia soma

Magazeti ya Kenya: Obasanjo awakutanisha Uhuru, Gachagua kuwachorea jinsi ya kumbwaga Ruto 2027

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilithibitisha kwamba mkutano huo ulifanyika Jumatatu, Februari 2, kufuatia notisi rasmi iliyotolewa Januari 29.

Msajili John Cox Lorionokou alisema muungano huo ulifuata taratibu zinazohitajika katika kuitisha Baraza la Azimio na Baraza Kuu la Muungano wa Kitaifa.

“Ofisi hii inakubali kupokea barua yako ya Februari 2 kwenye mkutano wa pamoja wa Baraza la Azimio na Baraza Kuu la Muungano wa Kitaifa mnamo Februari 2,” msajili alisema katika barua iliyoandikiwa uongozi wa muungano.

Kulingana na msajili, Junet Mohammed aliarifiwa rasmi kwa maandishi kuhusu kuondolewa kwake katika nafasi ya katibu mkuu.

Muungano huo ulishauriwa zaidi kutangaza mabadiliko katika muundo wake wa uongozi kulingana na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 7D, ambacho kinasimamia utawala wa ndani wa chama na uwazi.

Hii inakuja miezi kadhaa baada ya kifo cha kiongozi wa zamani wa Azimio Raila Odinga, ambaye aligombea urais chini ya muungano huo mwaka wa 2022 bila mafanikio.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *