Wasuluhishi kutoka Ukraine, Urusi na Marekani wanatarajiwa kukutana leo mjini Abu Dhabi, wakitafuta kuendeleza mazungumzo tete ya namna ya kumaliza vita vya karibu miaka minne.

Ujumbe wa Urusi tayari umewasili Abu Dhabi, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Moscow, ingawa haikuwa wazi kama wajumbe wa Marekani wamewasili huku wale wa Ukraine wakiwasili leo.

Duru kadhaa za kidiplomasia kati ya pande hizo zimeshindwa kufikia makubaliano ya kukomesha mzozo mbaya zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia, ulioanza wakati Urusi ilipoivamia Ukraine mnamo Februari mwaka 2022.

Wakati mazungumzo hayo yakisubiriwa, Urusi imeishambulia miundombinu ya umeme ya Ukraine kwa droni na makombora, na kusababisha kukatika kwa umeme katikati mwa msimu wa baridi kali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *