Watu wasiopungua  21 wanaripotiwa kuuawa na zaidi ya wengine 30 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya Israel huko Gaza siku ya Jumatano baada ya mapigano kuanza upya katika eneo hilo la pwani. Mamlaka ya afya inayoongozwa na Hamas imesema matukio hayo yalishuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza tangu alfajiri, jambo linaloonyesha kuyumba kwa makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas.

Jeshi la Ulinzi la Israel IDF, katika chapisho lake kwenye mtandao wa Telegram, limesema limefanya mashambulizi kadhaa kaskazini mwa Gaza baada ya magaidi kufyatua risasi dhidi ya wanajeshi wake na kumjeruhi vibaya afisa wa jeshi la akiba. Licha ya makubaliano ya kusitisha vita, kumekuwa na makabiliano makali huku kila upande ukimshutumu mwenzake kwa kukiuka makubaliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *