Abu Dhabi

Wajumbe kutoka Moscow na Kyiv wamekutana leo mjini Abu Dhabi kwa awamu nyingine ya mazungumzo yanayosimamiwa na Marekani kuhusu kumaliza vita vilivyodumu takribani miaka minne, wakati mabomu ya Urusi yakiwaua watu saba katika soko nchini Ukraine.

Mkuu wa Baraza la usalama wa kitaifa na ulinzi la Ukraine Rustem Umerov, ambaye amehudhuria mkutano huo, amethibitisha kukutana kwa wajumbe wa pande tatu. Hata hivyo Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema Moscow haiwezi kutoa maelezo juu ya mazungumzo hayo lakini inaendelea na operesheni yake hadi pale Kyiv itakapotimiza matakwa ya Urusi.

“Hadi maamuzi husika yatakapotolewa na utawala wa Kyiv, operesheni maalum ya kijeshi inaendelea. Jeshi letu linashambulia maeneo ambayo linaamini yanahusishwa na mfumo wa kijeshi wa utawala wa Kyiv. Operesheni inaendelea”, alisema Peskov.

Timu ya Marekani inajumuisha mjumbe maalum wa kanda ya Mashariki ya Kati Steve Witkoff na mkwe wa Rais Donald Trump, Jared Kushner.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *