Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu ameweka wazi kuwa ofisi yake haijapokea barua yoyote wala kutoa kibali kwa mbunge yeyote kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Ametoa kauli hiyo mapema leo bungeni wakati akieleza hali iliyojitokeza wiki iliyopita, kufuatia taarifa zilizosambaa kuwa baadhi ya wabunge waliitwa na TAKUKURU kutokana na maoni waliyoyatoa bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi