Wajuzi wa masuala ya maendeleo binafsi wanashauri kuwa ili kufanikisha malengo yako, ni muhimu kuwa na watu watakaokusaidia kusonga mbele katika maisha. Vijana wengi wanaita hilo “connection,” yaani mtandao wa watu wenye ujuzi, nafasi au uzoefu wanaoweza kukusaidia kufanikisha ndoto zako.
Mshahuri wa Maisha, Anthony Luvanda, anasema kuwa faida kubwa ya kuwa na connection ni kwamba inakuwezesha kupata ushauri sahihi, fursa za kibiashara, kazi au elimu, na pia kuondoa
vikwazo vinavyoweza kuzuia mafanikio yako.
✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri | John Mbalamwezi
#azamtvupdates