Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mauro Vieira, amesisitiza haja ya kuanzishwa mfumo mpya wa kimataifa unaotegemea marekebisho ya mashirika ya kimataifa yaliyopo, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama la umoja huo na Shirika la Biashara Duniani.

Mauro Vieira amesisitiza kwamba mageuzi ya mfumo wa kimataifa sasa ni jambo ambalo haliwezi kuepukwa.

Kuhusu suala la Venezuela, Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil amelaani tena utumiaji wa mabavu kumuondoa rais madarakani, akiutaja kuwa ni mfano hatari katika mahusiano ya kimataifa.

Ametilia mkazo kwamba kipindi cha mpito cha kisiasa nchini Venezuela lazima kitokane wa wananchi wenyewe.

Hapo awali, Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, alimshutumu mwenzake wa Marekani, Donald Trump kwa kutaka kuwa “bwana” wa “Umoja mpya wa Mataifa” kwa kuunda “Baraza la Amani la Gaza”.

Katika hotuba yake ya kuanza kazi Baraza la Amani, Lula da Silva alihoji: “Badala ya kurekebisha Umoja wa Mataifa, nini kinatokea? Rais Trump anapendekeza kuunda Umoja mpya wa Mataifa ambalo yeye atakuwa bwana pekee.”

Lula da Silva

Rais wa Brazil alielezea masikitiko yake kwamba “Mkataba wa Umoja wa Mataifa unavunjwa,” akitangaza kwamba ametumia “wiki moja kuwasiliana na nchi zote duniani” katika jaribio la “kutafuta njia ya kukutana” na kutetea mfumo wa kambi kadhaa.

Rais wa Brazil pia amekosoa Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa kwa kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akisema kwamba vyombo hivi havifanyi kazi yao ipasavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *