Katika taarifa iliyotolewa Februari 4, jijini New York, Marekani na Msemaji wake, Stéphane Dujarric, Katibu Mkuu ametoa rambirambi za dhati kwa familia za waliokumbwa na tukio hilo pamoja na wananchi na serikali ya Nigeria. Pia amewatakia majeruhi ahueni ya haraka.

Aidha, Katibu Mkuu amesisitiza mshikamano wa Umoja wa Mataifa na serikali ya Nigeria, pamoja na watu wa Nigeria katika juhudi zao za kupambana na ugaidi na itikadi kali za vurugu.

Ameeleza umuhimu wa wahusika wa shambulio hilo kufikishwa mbele ya sheria ili kuwajibishwa kwa vitendo vyao.

Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono juhudi za kimataifa na za kitaifa za kukabiliana na ugaidi, huku ukisisitiza haja ya kulinda raia na kudumisha amani na usalama.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa wanamgambo wenye msimamo mkali waliua zaidi ya watu 100 wakati waliposhambulia vijiji huko Woro na Nuku jimboni Kwara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *