KUTOKA ANGOLA: Angola ni miongoni mwa mataifa machache duniani yanayozungumza Kireno ikiwa ni lugha rasmi ya Taifa.
Kwa Afrika ni Guinea Bissau, Msumbiji, Angola na Cape Verde wanaotumia lugha hii kwenye mawasiliano.
Ahmed Ally ambaye ni Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC ni moja ya watu ambao wanapata shida hapa Angola kwenye mawasiliano kwani neno pekee analolifahamu ni Obrigado lenye maana ya “Shukrani kwa Mwanaume”
Simba ipo Angola kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Petro Atletico.
Mechi ni kesho saa 1:00 usiku LIVE #AzamSports2HD
#CAFCL #LigiYaMabingwaAfrika