KUTOKA ANGOLA: “Mazoezi ya leo ndio mazoezi ya mechi kabisa…”
Meneja habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally, alipozungumza jana na mwandishi wa #AzamTV @mangasore_ ambapo amebainisha kuwa mazoezi ya jana kwa timu hiyo yalibeba uhalisia wa mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Petro De Luanda.
Ahmed alisema mazoezi ya leo ijumaa yatakuwa ya mwisho kuweka miili ya wachezaji sawasawa.
#CAFCL #LigiYaMabingwaAfrika