
Wawakilishi wa Iran na Marekani leo wamefanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja mjini Muscat, Oman kuhusu mpango wa nyuklia wa amani wa Iran na kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Awamu ya pili ya mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyyed Abbas Araqchi na mwenzake wa Oman Sayyid Badr bin Hamad Al Busaidi imemalizika na wakati huo huo, mjumbe Maalumu wa Marekani Steve Witkoff pia ameanza mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman.
Mazungumzo ya nyuklia na kuondolewa vikwazo Iran kati ya Tehran na Washington yamefanyika leo, Ijumaa, Februari 7, huko Muscat, mji mkuu wa Oman, kwa upatanishi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo.
Ajenda kuu ya mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja ni faili la la nyuklia la Iran na kuondolewa vikwazo taifa hili vilivyowekwa na Marekani.
Oman imekuwa na jukumu kubwa kama mpatanishi kati ya nchi za kikanda katika miaka ya hivi karibuni, na mazungumzo ya leo inaonekana kama mwendelezo wa mpango wa kidiplomasia wa nchi hii wa kupunguza mvutano katika eneo hilo.
Taarifa zaidi kuhusiana na natija ya mazungumzo ya leo hazijatolewa.
Kabla ya kluanza mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi alisema Tehran inaingia katika duru mpya ya mazungmzo ya kidiplomasia na Marekani ikiwa hadhiri, makini kabisa na “kwa macho yaliyo wazi.”
Waziri Araghchi alisisitiza kwamba, Iran ina “kumbukumbu thabiti ya mwaka uliopita” katika mazungumzo, akiashiria tahadhari iliyochochewa na uzoefu wa huko nyuma. Huku akisisitiza utayarifu wa Iran wa kufungamana na diplomasia, ameeleza bayana kwamba, Tehran “itasimama kidete kutetea haki zake.”