Katika makazi ya muda ya mpaka wa Am Dafock Birao wakimbizi wanapokea msaada wa chakula kutoka kwa WFP. Tangu Novemba mwaka jana, Shirika hilo la Mpango wa Chakula Duniani, lilianzisha operesheni ya dharura mjini Am Dafock eneo lililotengwa kutokana na ukosefu wa usalama na miundombinu mibovu ambako vurugu zinazosambaa kutoka Sudan zimesababisha familia nyingi kukimbia makazi yao.

Kutokana na ukosefu wa njia salama za ardhini, chakula kimelazimika kuletwa mjini hapa kwa njia ya anga. Aurore Vinot, ni Mtaalamu wa vyombo vya habari na afisa wa mawasiliano wa WFP anasema

“Am Dafock, mbali na changamoto za kiusalama na vurugu zinazolikumba eneo la mpakani na Sudan, ni eneo gumu sana kufikika. Hivyo, usafiri wa anga ulikuwa ndio njia pekee ya kuwapatia watu msaada unaohitajika.”
Daraja hilo la anga liliwezesha kufikiwa kwa zaidi ya watu 12,000 waliokumbwa na mzozo, wakiwemo wakimbizi wa ndani na watoto walio katika hatari ya utapiamlo.

WFP imegawa Biskuti zenye nguvu pamoja na chakula maalum cha lishe ukiwa ni msaada muhimu kwa familia ambazo zimekuwa bila chakula cha uhakika kwa wiki kadhaa sasa.
Operesheni hii imefanyika kwa ushirikiano na ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini CAR ujulikanao kama MINUSCA, ili kuhakikisha usafirishaji salama wa msaada hadi katika eneo hili la mpakani lililotengwa.

Aurore Vinot, ameongeza kuwa “Operesheni ya dharura Am Dafock, iliyoongozwa na WFP, imeenga kusaidia watu walio katika mazingira magumu na waliokimbia makazi yao mpakani na Sudan. Ni eneo gumu sana kufikika. Na kutokana na uratibu na MINUSCA, tumeweza kusafirisha na kugawa zaidi ya tani 20 za chakula na virutubisho vya lishe kwa kituo cha afya.”

Zaidi ya tani 20 za chakula na virutubisho vya lishe sasa zimefika kwa jamii hiyo ya wakimbizi ambao ni msaada wa kuokoa maisha katika eneo ambalo migogoro,

WFP inasema ufikiaji endelevu wa maeneo athirika na ufadhili wa kutosha ni muhimu ili kuendeleza msaada Am Dafock, wakati hali ya ukosefu wa usalama mpakani na Sudan ikiendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *