Trump amesaini dikrii kwa ajili ya kuwatoza ushuru washirika wa kibiashara wa Iran.
Kwa mujibu wa ripoti ya Pars Today, Rais Donald Trump wa Marekani jana aliendeleza sera zake za undumakuwili mkabala wa Iran na kusaini dikrii ambapo amezitosha ushuru wa asilimia 25 nchi ambazo zinafanya biashara na Iran mbali na ushuru wa awali alioutangaza. Trump amechukua hatua hii licha ya kufanyika duru mpya ya mazungumzo kati ya Tehran na Washington.
Kwa mujibu wa dikrii hiyo ambayo imeanza kutekelezwa tangu jana Jumamosi Februari 7; Marekani itazitoza ushuru wa pili nchi washirika wa kibishara wa Iran. Uamuzi huu unamaanisha kwamba katika hali ambayo wananchi wa Iran wanakabiliwa na vikwazo vikali sambamba na mashinikizo ya kiwango cha juu Trump anadai kuwa anawaunga mkono; ;na Iwapo nchi yoyote inataka kuendelea kufanya biashara na Iran, itakabiliwa na adhabu mpya ya ushuru wa Marekani.
White House pia imeidhinisha kusainiwa dikrii hiyo na Trump na kutangaza kuwa, kwa mujibu wa dikrii hiyoMarekani inaweza kuzidisha ushuru wa ziada kwa bidhaa zote zitakazoingizwa na nchi ambazo zinanunua bidhaa au huduma moja kwa moja au kwa njia isiyo moja kwa moja kutoka Iran.
Dikrii hii ambayo imeratibiwa katika sehemu tisa tofauti imetegemea mamlaka ya Rais ndani ya Katiba ya Marekani na Sheria ya Mamlaka ya Kiuchumi katika Mazingira ya Dharura Kimataifa. Tangu dikrii hii tajwa itakapotekelezwa; kiwango cha ziada cha ushuru wa forodha (kwa mfano, asilimia 25) kitatumika kwa bidhaa zote zinazoingia Marekani kutoka nchi zinazonunua bidhaa au huduma za Iran. Mchakato wa utekelezaji umeratibiwa kwa namna ambayo awali Wizara ya Biashara ya Marekani inapasa kuzitambua ni nchi zipi zinazofanya manunuzi moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka Iran. Baada ya kuthibitishwa hilo, Wizara ya Mambo ya Nje, kwa kushirikiana na Idara za Hazina, Biashara, Usalama wa Nchi na Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, itabainisha kiwango na ukubwa halisi wa ushuru na kutoa pendekezo la mwisho kwa Trump kwa ajili ya kuanza utekelezaji. Iwapo itatokea nchi ikachukua hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya Marekani katika kukabiliana na ushuru huu tajwa, Rais wa Marekani ana mamlaka ya kuongeza ushuru zaidi au kutekeleza hatua mpya za adhabu dhidi ya nchi hiyo.
Katika hatua nyingine dhidi ya Iran; Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani sambamba na kufanyika duru mpya ya mazungumzo kati ya Tehran na Washington imewawekea vikwaz vipya vya mafuta shakhsia 17 na taasisi na meli 14. Ikikariri madai yake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Washington imedai kuwa inawawekea vikwazo shakhsia, taasisi na meli kadhaa ili kusitisha mtiririko wa mapato kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kutiwa saini na Donald Trump dikri mpya ya utekelezaji kwa ajili ya kutoza ushuru wa adhabu (kama vile kiasi cha asilimia 25) kwa nchi zinazofanya biashara na Iran ni hatua ya pande kadhaa iliyochukuliwa katika fremu ya malkengo ya kimkakati ya Marekani. Kwa upande wa kimkakati; lengo lililotangazwa ni kukamilisha mzingiro wa kiuchumi wa Iran kwa kutekelezwa vikwazo vya pili na kupunguza mapato ya mafuta ya Iran hadi sifuri. White House imeashiria “dharura ya kitaifa” na kuitaja hatua hii kuwa hatua ya dharura kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa na maslahi ya Marekani mkabala wa kile ilichokitaja kuwa ” tshio lisilo la kawaida” la Iran kupitia miradi yake ya nyuklia na makombora na uungaji mkono wake kwa makundi ya niaba katika eneo. Nukta muhimu hapa ni hii kuwa mashinikizo hayaelekezwi tu moja kwa moja kwa Iran, bali pia kwa mtandao wake wa washirika wa kibiashara, na hivyo kuongeza pakubwa gharama ya kufanya biashara na Tehran.
Kwa upande wa mbinu, muda wa kutiwa saini dikrii hii, ambako kumejiri sambamba au mara tu baada ya kumalizika duru mpya ya mazungumzo ya Iran na Marekani huko Muscat, una umuhimu. Kujiri kwa wakati mmoja masuala haya inatafsiriwa kama kiwango cha kuzidisha mashinikizo na kuwa na nafasi nzuri Washington; na inatuma ujumbe wa wazi kwamba sera ya mashinikizo ya kiwango cha juu itaendelea bila kujali mazungumzo. Trump binafsi amesisitiza baada ya mazungumzo kwamba “matokeo mazito sana” yanaisubiri Iran iwapo haitafikia mapatano.

Kwa upande wa utekelezaji, dikrii hii inaunda utaratibu tata. Awali, Wizara ya Biashara ya Marekani inapasa kuzitambua nchi zinazonunua bidhaa kutoka Iran. Kisha Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo kwa kushirikiana na idara kama Hazina, ndizo zitakazoainisha kiwango sahihi cha ushuru kutoa mapendekezo kwa Rais. Mwenendo huu unaipa Marekani uwezo wa hatua kwa hatua kuzidsha mashinikizo kulingana na radiamali na majibu yatakayotolewa na nchi mbalimbali mkabala wa hatua zake hizi. Pia kuna kifungu katika utaratibu huo ambacho kinampa Rais mamlaka ya “kurekebisha” amri ikiwa mazingira yatabadilika, nchi zitalipiza kisasi, au ikiwa Iran au washirika wake watachukua “hatua muhimu” ili kwenda sambamba na Washington. Kifungu hiki ni wenzo wa adhabu na wakati huo huo inazifanya nchi zikubali na kusalimu amri mbele ya matakwa ya Washington.
Kiujumla, hatua hii inaweza kutajwa kama jitihada za kubadilisha vikwazo vya awali vya Marekani dhidi ya Iran kuwa mzingiro wa pande zote wa kiuchumi na kimataifa. Lengo la mwisho, kuitenga zaidi Iran, kuweka vikwazo vikali kwa rasilimali za fedha za Iran na kuilazimisha Tehran au washirika wake wa kibiashara kukubali masharti ya Washington kwa kuwa na chaguo gumu kati ya kuamua kufanya biashara na Iran au kufikia soko kubwa la Marekani.
Pamoja na haya yote, Iran kama ambavyo katika duru ya kwanza ya urais wa Trump iliweza kupambana kukabiliana na na hatua za uhasama za Washington ili kupunguza mauzo yake ya mafuta na kufikisha mapato yake hadi sifuri licha ya kutekelezwa sera za mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi yake; mara hii pia kwa kuzingatia kukataa wazi mshirika muhimu zaidi wa kibiashara wa Iran yaani China kukubali matakwa ya Washington kunaweza kwa mara nyingine tena kufelisha sera za Trump dhidi ya Iran.