Shirikisho la mpira wa miguu barani afrika kupitia kamati tendaji inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wake mnamo tarehe 13 mwezi huu, jijini Dar Es Saalam ambao utajadili masuala mbalimbali ya Maendeleo ya mchezo wa soka hapa nchini.
Akitangaza Taarifa hiyo waziri wa wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo Paul Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari za michezo ambapo amesema kuwa mkutano huo kufanyika hapa nchini ni kutokana na uwekezaji mkubwa wa serikali katika sekta ya michezo kuanzia miundombinu na timu mbalimbali za taifa.
(Feed generated with FetchRSS)