
Baraza la Mawaziri nchini Israel, limepitisha hatua za kuchukua maeneo zaidi na kutawala katika Ukingo wa Magharibi inayokalia kimabavu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii itasababisha uuzwaji wa ardhi ya Wapalestina, kwa walowezi wa Israel, ikiwa na maana kuwa Israel sasa itatawala hadi katika eneo hilo la Palestina.
Hatua hii imelaaniwa na rais wa mamla ya Palestina Mahmoud Abbas, ambaye amesema kitendo hicho cha Israel ni hatari na kinyume cha sheria.
Aidha, Abbas amemtaka rais wa Marekani Donald Trump na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati, kitendo hicho alichosema ni Israel kuchukia kwa nguvu, ardhi ya Wapalestina.
Jordan imeshtumu kitendo hicho ilichosema, Israel inalazimisha utawala wake kwa nguvu na kuanzisha makaazi ya walowezi kwa nguvu, shutuma ambazo pia zimetolewa na Umoja wa Ulaya kupitia msemaji wake Anouar El Anouni, ambaye amesema hatua hiyo ya Israel haifai.