
Mkasa huo umetokea Tumbler Ridge, mji wenye watu 2,300 katika jimbo la British Columbia, zaidi ya kilomita 1,000 kaskazini mashariki mwa Vancouver. Mshukiwa wa mauaji hayo pia amepatikana amekufa, kufuatia jeraha alilojisababishia mwenyewe.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tukio hili katika shule ya upili na makazi ya karibu liligharimu maisha ya watu tisa siku ya Jumanne, Februari 10, katika eneo la mbali magharibi mwa Canada, polisi imesema, huku ikiongeza kuwa mshambuliaji amepatikana amefariki. Shambulio hilo lilitokea Tumbler Ridge, mji mdogo wenye watu 2,300 katika safu ya milima iliyopo katika nyanda za juu katika jimbo la British Columbia.
Jumla ya watu 27 walijeruhiwa, wawili vibaya na wengine 25 wakiwa na majeraha madogo, Polisi wa kifalme wa Canada wamesema katika taarifa. Kulingana na vyombo kadhaa vya habari vya Canada, mshambuliaji alikuwa mwanamke, lakini polisi, ambayo ilifanya mkutano na waandishi wa habari baadaye siku hiyo, ilikataa kutoa maelezo yoyote kuhusu utambulisho wa mshukiwa.
Mauaji ni nadra nchini Canada, lakini hili ni tukio la pili huko British Columbia katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja. Mnamo mwezi Aprili 2025, watu kumi na mmoja waliuawa huko Vancouver wakati mtu mmoja alipoendesha lori lake na kuingia kwenye umati wa watu waliokuwa wakisherehekea tamasha la kitamaduni la Ufilipino.
Kulingana na taarifa za awali za polisi, tahadhari ya kwanza iliyopokelewa alasiri ilimhusu mshambuliaji aliyekuwa akifanya kazi katika Shule ya Upili ya Tumbler Ridge. Walipofika, maafisa walipekua shule na kugundua watu sita waliouawa, pamoja na mshukiwa. Mtu wa saba aliyepigwa risasi shuleni alifariki alipokuwa akisafirishwa kwenda hospitalini. Polisi baadaye “waligundua eneo la pili linaloshukiwa kuhusishwa na tukio hilo, ambapo waathiriwa wengine wawili walipatikana wamefariki katika makazi,” kulingana na taarifa. Mshukiwa anaripotiwa kufariki kutokana na “jeraha alilojisababishia mwenyewe.”
Waziri Mkuu Mark Carney “asikitika”
Katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Waziri Mkuu Mark Carney amesema “amehuzunishwa” na “tukio hilo baya.” “Ninaungana na Wacanada kutoa rambirambi zangu kwa wale ambao maisha yao yamekatizwa leo, na pongeza ujasiri na kutojitoa kwa waokoaji wa kwanza waliohatarisha maisha yao ili kuwalinda raia wenzao,” ameongeza.
“Hili ni jambo ambalo wegi tulifikiri halitatokea kamwe,” Shelley Quist, mkazi wa Tumbler Ridge na mama wa mwanafunzi shuleni hapo, aliambia kituo cha habari cha serikali cha CBC. “Sitamwondolea macho kwa muda sasa,” ameongeza, akimrejelea mwanawe Darian, ambaye yuko salama salimini.
Mchana, tukio hili baya liliwalazimu wakazi wa Tumbler Ridge na eneo jirani kusalia katika nyumba zao. Mji huo unajulikana kwa utalii wake wa nje, ukiwa karibu na milima na bustani ya kijiolojia. Alasiri, polisi “walimaliza tahadhari ya dharura huko Tumbler Ridge.” Polisi haiamini kwamba kuna washukiwa wowote waliokimbia au tishio lolote kwa umma,” Waziri wa Usalama wa Umma wa jimbo hilo amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X.