
Baraza la Seneti nchini Marekani limepitisha azimio siku ya Jumanne, Juni 23, likiamuru kuondolewa kwa vikosi vya Marekani kwenye mgogoro na Iran. Hili kimsingi ni pigo kubwala kishara kwa Donald Trump, kwani azimio hilo halitakuwa la kisheria.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baraza la Seneti nchini Marekani limepitisha azimio siku ya Jumanne, Juni 23, likiamuru kuondolewa kwa vikosi vya Marekani katika mzozo na Iran. Hili kimsingi ni pigo la kiishara kwa Donald Trump, ambaye amelaani muswada huo, akisema hautakuwa na nguvu ya kisheria.
Duru ya kwanza ya mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Iran ilimalizika siku ya Jumatatu nchini Uswisi. Iran, kwa upande wake, ilisisitiza nia yake ya kudumisha udhibiti wa Mlango-Bahari wa Hormuz, licha ya tangazo la Washington la kuondoa vikwazo dhidi ya mafuta ya Iran kama sehemu ya mazungumzo haya yenye lengo la kukomesha vita katika Mashariki ya Kati.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alikataa hoja ya Iran kuendelea kutoza ushuru au ada kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz.
Lakini kura hii inawakilisha kikwazo kwa rais wa Marekani kutoka chama cha Republican, ambaye yuko katikati ya mazungumzo na Iran na ambaye chama chake kinashikilia wingi katika mabunge yote mawili. “Kwa hivyo, Iran inaelea majini, iko karibu ya kudidimia (…) na Baraza la Seneti la Marekani linaamua kufanya kura kwa wakati usio muafaka na isiyo na maana kuhusu Sheria ya Mamlaka ya Vita,” alisema siku ya Jumanne jioni kwenye jukwaa lake la Truth Social, akiwashutumu maseneta kwa “kufanya mambo kuwa magumu kwake” na “kutoa msaada na faraja kwa adui.”
Muswada huo ulipopitishwa katika Baraza la Wawakilishi mapema mwezi huu, alilaani kura ya “kutokuwa na uzalendo” ya upinzani wa Democratic na wawakilishi wanne wa Republican waliojiunga nao. Wademocrats”wangependelea kuona nchi yetu ikishindwa kuliko kunipa ushindi mwingine,” alisema wakati huo. Kwa wiki nyingi, upinzani umekuwa ukijaribu kuzuia mamlaka ya kijeshi ya Donald Trump katika mzozo na Iran, ukishutumu serikali yake kama inakiuka maazimio yanayopitishwa an Mabunge yote mawili.