Tunaelekea  Beni mashiriki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambako George Musubao kutoka Televishen na Radio washirika Canal Victoire Du People Kasindi, amezungumza na mwana habari na mtangazaji wa Redio kubaini zaidi

Beni, mji ulio karibu na mbuga ya wanyama ya Virunga, jimboni Kivu Kaskazi ni makazi ya Luhemwe Erickson, mwandishi wa habari kwenye kituo cha redio cha Top Congo FM.

Redio na akili mnemba AI

Kwanza Erickson anaeleza akili mnemba inamusaidiaje katika kazi yake ya uandishi wa habari hapa mashariki mwa DRC.

 ” Nina taarifa kuhusu Akili Mnemba. Ninawaona watu wakiitumia lakini mimi binafsi sijawai itumia kwasababu mimi ninafanya kazi kwenye redio isiyotumia mfumo wa Akili Mnemba, sio kwamba kutoitumia haifanye kazi. Ndio inafanya kazi kwa baadhi ya watu lakini mimi kazi ninaoifanya haitaji zaidi mfumo wa Akili Mnemba”

Bwana Erickson akifafanua zaidi anazungumzia tofauti kati ya habari za moja kwa moja za redio na zile zinazotolewa na teknolojia ya Akili Mnemba.

Mwalimu anarekebisha sauti ya spika iliyounganishwa na simu ya mkononi ili wanafunzi waweze kufuatilia kipindi cha elimu huko DRC.

Mwalimu anarekebisha sauti ya spika iliyounganishwa na simu ya mkononi ili wanafunzi waweze kufuatilia kipindi cha elimu huko DRC.

” Habari ambazo ninazipata kupitia redio nina imani nazo zaidi kwasababu kwenye redio ikiwa topiki inayohusu siasa nitamsikiliza mwanasiasa kutoka kambi ya upinzani lakini pia mwanasiasa kutoka kambi tawala. Tofauti na Akili Mnemba nina imani zaidi kwa habari zinazotolewa na redio kuliko habari ninazo zipata kupitia Akili Mnemba. Kwa njia ya redio ni raisi kufaamu kwamba aliyeongea ni nani ikiwa ni mambo yanayohusu siasa au mazingira nitamujua mtaalamu nimemuona na amezungumza kwa sauti yake na huku kama ni siasa nitajua huyu ametoka kambi ya upinzani na ninamfahamu”.

Faida na changamoto za AI

Leo, Akili Mnemba (AI) inafungua sura mpya kuimarisha uhusiano na wasikilizashi. Ina pande mbili za shilingi, faida na changamoto, sasa Erickson Luhembwe anazungumzia changamoto kufuatia matumizi mabaya ya AI hasa nchini DRC.

” Wazo lenyewe la Akili Mnemba vifaa vyake vimeundwa kwa ajili ya kazi lakini wasiokua katika sekta ya uhandishi wa habari wanaitumia vibaya. Changamoto ni nyingi, mfano taarifa potofu, mathalani hivi karibuni siku mbili zilizopita picha ya aliyekua raisi wa Congo ilisambazwa kusema kwamba atahutubia, watu wamepoteza muda murefu  kuchunguza kama ni habari la ukweli lakini baadae tulipoichunguza na vyombo vya habari pia na TV imekutwa kwamba picha hiyo ilitengenezwa na Akili Mnemba. Ndio maana huo mfumo unachukua muda kwa watazamaji na kwa wasikilizaji kuanza kuchunguza kama habari ni potofu ya uongo kuliko kupokea habari ilikujua kuendekea vipi na maisha kawaida nchini ao kitaifa“(Hapa sijaelewa unasema nini?)

Mwanamke katika cardigan ya kijivu akibeba kipaza sauti wakati wa mahojiano ya nje kwa ajili ya Siku ya Redio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Marie Kahashi, msikilizaji wa redio. Yeye ni mkazi wa Beni anayefahamu kuhusu AI.

AI na ujasiriamali

Marie Kahashi yeye ni mkazi wa Beni anayefahamu kuhusu AI hapa anazungumzia umuhimu wa redio na AI katika kazi yake na kufikia malengo yake. Akisema projet anamanisha mradi na entrepreneuriat anamaanisha kazi za ujasiriamali

” Nina uzoefu kusikiliza redio na zaidi sana vipindi vya habari kuhusu usalama, mambo ya jamii pia na kuhusu mazingira, ni hayo ndio nina uzoefu kusikiliza. Nina maarifa kuhusu Akili Mnemba mimi zaidi naitumia ChatGPT nikifanya utafiti kujifunza kwani napenda sana entrepreneuriat, kazi ya mukono, najifunza pia namna gani ya kuanzisha mradi fulani na namna gani kuifikia, vipindi gani vya kupitia ili nifikie kwenye miradi inaohusu kazi za mkono”.

Bi. Marie akatoa wito kwa Umoja Wa Mataifa. Akisema conditions anamaanisha mazingira, na confiance anamaanisha tumaini.

” Nina ombi kwa Umoja Wa Mataifa ni kwa sababu kwa sasa redio imeonekana inasahaulika kwa ajili ya kuja kwa Akili Mnemba na mitandao ya kijamii watu wanategemea sana zaidi huku wakitupilia mbali redio, si kwasababu hawapendi lakini ni kwasababu redio imeachwa na kazi haiendeki vizuri, waandishi wa habari hawasidiwi kufanya kazi katika mazingira yanayofaa. Lakini Umoja Wa Mataifa labda wakifanya miradi kusapoti redio hiyo itarejesha (confiance) matumaini kwa wakazi na wataweza kuamini tena kazi inaofanyika  kupitia redio”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *