Ugaidi na itikadi kali vinaendelea kuwa tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia, huku vikigusa watu wa rika, dini na tamaduni mbalimbali na ndio maana Umoja wa Mataifa unasema ingawa teknolojia kama akili mnemba au AI, mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali inaweza kusaidia juhudi za kuzuia misimamo mikali, pia inatumiwa na magaidi kueneza chuki, upotoshaji na kuhamasisha vurugu. 

Kutokana na hali hiyo ndio maana Umoja wa Mataifa unahimiza ushirikiano wa kimataifa, matumizi ya teknolojia kwa uwajibikaji na suluhisho shirikishi zinazoheshimu haki za binadamu ili kuzuia kuenea kwa itikadi kali.

Siku hii inalenga kuzikutanisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia, viongozi wa dini, sekta binafsi, wanataaluma na vyombo vya habari ili kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kuongeza uelewa kuhusu hatari ya misimamo mikali na kuimarisha hatua za kuizuia.

Maadhimisho ya siku hii yanafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Unaweza kufuatilia maadhimisho hayo mubashara hapa

Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa teknolojia si tatizo lenyewe bali matumizi yake. 

Kusoma zaidi kuhusu siku hii tembelea wavuti maalum wa siku hii hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *