Muigizaji Kanbolat Görkem Arslan, maarufu kwa uhusika wake kama Savcı Bey kwenye tamthilia ya OTTOMAN inayoruka Jumatatu hadi Ijumaa kupitia AzamTWO, amefariki dunia Jumanne wiki hii Februari 10, 2026 akiwa na umri wa miaka 45.

Taarifa za kifo chake zimethibitshwa na mwandaaji wa tamthilia za OTTOMAN na ERTUGRUL Mehmet Bozdağ, ambaye ameeleza kwamba Arslan amefariki kufuatia maradhi ya moyo; na kwamba anaungana na familia na mashabiki zake wote katika kipindi hiki kigumu.

Amezaliwa Novemba 4, 1980 mjini Düzce Uturuki, ni msomi wa masuala ya filamu kutoka Chuo Kikuu Cha Theatre Department at Hacettepe. Alianza safari yake ya sanaa mwaka 2004 aliposhiriki kwenye tamthilia maarufu ya Çemberimde Gül Oya.

#Savcibey #KanbolatGörkem

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *