
Bunge la Ulaya limepitisha azimio kuhusu hali ya baada ya uchaguzi nchini Uganda. Siku ya Alhamisi, Februari 14, 2026, Wabunge wa Umoja wa Ulaya walipiga kura kuunga mkono nakala inayolaani ukandamizaji dhidi ya upinzani, mahirika ya kiraia, na vyombo vya habari kufuatia uchaguzi wa urais wa Januari 15, na kutoa wito wa uchunguzi huru kuhusu madai ya ukiukwaji. Nakala hiyo, iliyopitishwa na idadi kubwa ya wabunge, imeibua hisia chanya kutoka kwa upinzani nchini Uganda.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa kura 514 zilizounga mkono, 3 zilizopinga, na wabge 56 waliojizuia, kura hiyo ilikuwa ya uamuzi. Ilikuwa azimio la pamoja, lililoungwa mkono na makundi kadhaa ya kisiasa.
Wabunge wa Umoja wa Ulaya walilaani “matusi, vitisho, ulaghai, na vurugu,” pamoja na kuimwa kwa huduma intaneti kote nchini, ambapo wanaamini kuliharibu mwenendo wa uchaguzi wa Januari 15. Pia walielezea wasiwasi wao kuhusu vitisho dhidi ya upinzani, hasa Bobi Wine na Kizza Besigye, na kulaani hatua ya kusitishwa mashirika ya mashirika ya kiraia.
Azimio hilo pia linatoa wito wa kuachiliwa huru mara moja na bila masharti kwa wale waliokamatwa kiholela, linalaani mauaji ya msaidizi wa NUP Mesach Okello, na linahimiza Kampala kuacha kuwashtaki raia katika mahakama za kijeshi. Hatimaye, wabunge wa Umoja wa Ulaya wanautaka Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wake kupitia ushirikiano wao na Uganda na kudai uchunguzi huru kuhusu uhalifu unaowezekana dhidi ya binadamu unaohusisha maafisa wa kisiasa na kijeshi.
Katika upinzani, Bobi Wine amekaribisha nakala hiyo kama “muhimu sana.” “Ulimwengu unaangalia,” ameandika, akielezea matumaini yake kwamba siku moja, “ukweli utashinda.”