Msemaji wa serikali ya Afghanistan amesisitiza kwamba watu wa Afghanistan wataonyesha mshikamano na kutoa aina mbalimbali za misaada kwa Iran iwapo kutatokea uchokozi wowote dhidi ya nchi hiyo.

Zabihullah Mujahid, amesema kwamba iwapo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itafanyiwa uchokozi wa aina yoyote, “watu wa Afghanistan watashikamana na kutoa aina mbalimbali za misaada kwa ndugu zao wa Iran.”

Mujahid aliyekuwa akizungumza jana mjini Kabul aliongeza kwamba Iran imeshinda Vita vya Siku 12, akisisitiza kwamba ina uwezo wa kushinda na kujilinda dhidi ya uchokozi wa aina wowote.

Wiki iliyopita, balozi wa Iran nchini Afghanistan, Ali Reza Bikdeli, alithibitisha kwamba nchi yake inaelekea kwa kasi katika kuimarisha uhusiano wake na Kabul katika nyanja mbalimbali, akieleza kuwa hakuna kinachozuia Tehran kutambua rasmi serikali ya Taliban, na kwamba utambuzi huo utafanyika hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *