Mkutano wa kimataifa kuhusu Akili Bandia (AI) umefunguliwa leo Jumatatu jijini New Delhi kujadili athari za mapinduzi yanayokuja, kuanzia ajira hadi ulinzi wa watoto, lakini washiriki wana shaka kwamba utatoa hatua madhubuti.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakuu zaidi ya ishirini wa nchi na serikali (Ufaransa, Brazil, Uholanzi, Uhispania, Falme za Kiarabu, n.k.) wanatarajiwa kujiunga na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa mkutano huu wa nne kuhusu teknolojia ambayo tayari inabadilisha jamii.

Wadau wengi wakuu wa tasnia hiyo pia wanatarajiwa katika mji mkuu wa India hadi Ijumaa, kuanzia Sam Altman, mkuu wa OpenAI, hadi Mkurugenzi Mtendaji wa Google, Sundar Pichai, na Jensen Huang, Mkurugenzi Mtendaji wa Nvidia, kampuni kubwa ya Marekani ya microprocessor.

“Mkutano huu utaimarisha mawazo ya kimataifa kuhusu vipengele mbalimbali vya AI, kama vile uvumbuzi, ushirikiano, na matumizi yake ya uwajibikaji,” Narendra Modi amesema kwenye mtandaowa kijamii wa X.

Pia ni “uthibitisho kwamba nchi yetu inapiga hatua za haraka katika uwanja wa sayansi na teknolojia” na “inathibitisha uwezo wa vijana wa taifa letu,” ameongeza.

Miongoni mwa mada zingine, warsha na mijadala ya kwanza iliyofanyika Jumatatu ilizungumzia uwezo wa AI kuboresha usalama barabarani nchini India na michango ya wanawake wa Asia Kusini katika sekta ya teknolojia.

– “Udhibiti mzito” –

Yakichochewa na utendaji mzuri wa soko la hisa la makampuni ya teknolojia, mapinduzi yanayoendelea yanaibua wasiwasi kuhusu athari zake kwenye mazingira, ajira, ubunifu wa kisanii, elimu, na habari.

Bado haijabainika ikiwa hatua za kisheria zitachukuliwa kudhibiti matumizi yake na kuzilazimisha kampuni kubwa katika sekta hiyo, anahoji Amba Kak, mkurugenzi mwenza wa Taasisi ya AI Now.

Hadi leo, ahadi zilizotolewa “zimepunguzwa katika kuanzisha mifumo ya ‘kujidhibiti kidogo,'” anabainisha mshauri huyu wa zamani wa AI kwa Tume ya Biashara ya Shirikisho la Marekani.

“Sekta ya AI inaendesha sio tu teknolojia yenyewe, bali pia jinsi tunavyoidhibiti (…) au la,” anasema.

Kufuatia “Mkutano wa Vitendo kuhusu AI” uliofanyika Paris mwaka jana, nchi kadhaa zilisaini tamko la AI ilio “wazi,” “jumuishi,” na “ya kimaadili”.

Marekani na Uingereza zimekataa kufanya hivyo, huku Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance akionya dhidi ya “kanuni nyingi” ambazo zinaweza “kuua tasnia inayostawi.”

Kwa mtaalamu wa Marekani Amba Kak, kama ilivyo kwa wataalamu wengine, mada zilizochaguliwa kwa ajili ya majadiliano huko New Delhi—”watu, maendeleo, na sayari”—ni haba sana kutumaini hatua madhubuti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *