Samia aibuka kinara AU kuboresha afya ya mama na mtotoSamia aibuka kinara AU kuboresha afya ya mama na mtoto

UMOJA wa Afrika (AU) imemthibitisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwa Kinara wa Afya ya Mama na Mtoto barani Afrika, kufuatia mafanikio makubwa ya kupunguza vifo vya kina mama na watoto kwa takribani asilimia 80.

Wakizungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Seif Shekalaghe, wamesema mwaka 2016 kiwango cha vifo vya kina mama kilikuwa 556 kwa kila vizazi hai 100,000, lakini kufikia mwaka 2022 kimepungua hadi 104 kwa kila vizazi hai 100,000.

Mafanikio hayo yamechangiwa na kuimarishwa kwa huduma za msingi za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, pamoja na ongezeko la bajeti ya sekta ya afya.Utambuzi huo ni matokeo ya mageuzi ya kimkakati katika sekta ya afya yaliyowekwa na kusimamiwa chini ya uongozi wake, yakilenga kuboresha huduma za uzazi, upatikanaji wa wataalamu na miundombinu ya tiba nchini. SOMA: “Tumeboresha afya ya uzazi, mama na mtoto”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *