#HABARI: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema imeimarisha Dawati la Huduma kwa Wateja na mifumo ya ufuatiliaji wa watoa huduma, hatua inayolenga kuongeza uwazi, ufanisi na ushirikishwaji katika maamuzi ya sekta ya mawasiliano.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, amesema maboresho hayo yameweka mazingira wezeshi kwa watoa huduma kushiriki kikamilifu katika michakato ya maamuzi na utoaji wa maoni.
Dkt. Bakari amefafanua kuwa kupitia Dawati la Huduma lililoboreshwa, wadau wanaweza kuwasilisha hoja, changamoto na mapendekezo yao kwa urahisi na haraka zaidi, huku mifumo ya Kidijitali ya ufuatiliaji ikihakikisha mawasiliano yanakuwa ya wakati na yenye tija.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
Powered by MCHEZOSUPA