Waumini wa dini ya Kiislamu nchini kesho wanaungana na Waislamu wengine duniani kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya kukamilika kwa mwezi wa Shaaban.

Taarifa zilizotufikia hivi punde na zilizotangazwa na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar bin Zubeir bin Ally Mbwana kutoka Korogwe mkoani Tanga, zimesema mwezi umeonekana maeneo mbalimbali nchini ikiwemo eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam, hivyo kesho ni Ramadhan.

Mufti Zuberi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mwezi, amesema kamati yake imejiridhisha na taarifa za mwandamo wa mwezi na ametumia fursa hiyo kuwatakia heri na baraka waislamu katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *