Kigoma. Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma limesema linafanya uchunguzi wa taarifa za kutoweka kwa mfanyabiashara wa soko la Buzebazeba, Mahamoud Abdallah (25) na mkazi wa kata ya Mwasenga, Manispaa ya Kigoma Ujiji, akidaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma jana Februari 20, 2026, mfanyabiashara huyo alidaiwa kutoweka katika eneo lake la kazi na tukio hilo kuripotiwa Februari 19, 2026 saa 3:00 asubuhi.

Taarifa hiyo imesema uchunguzi utakapokamilika utabaini ukweli wa tuhuma hizo na kwamba, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linatoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa au ushahidi ambao utasaidia uchunguzi kukamilika kwa wakati aufikishe Polisi ili uweze kufanyiwa kazi kwa haraka.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, linaendelea kuwaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo na hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya wahusika,” imesema taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *