
Tukio hilo lilitokea usiku wa Jumapili, Februari 8, lakini liligunduliwa siku ya Ijumaa, Februari 20. Shirika la ndege la Air Côte d’Ivoire, lilikuwa mwathiriwa wa shambulio hilo la mtandaoni. Kulingana na taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo, ilihusisha ” udukuzi wa faili zenye data nyeti.” Ingawa shambulio hili la mtandaoni halikuvuruga shughuli za anga, maswali yanabaki kuhusu usalama, haswa kuhusu data za abiria.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Abidjan, Abdoul Aziz Diallo
“Ni shambulio la wizi wa data, ransomware,” chanzo ndani ya shirika la ndege la Air Côte d’Ivoire kimekiri. Kwa maneno mengine, programu hasidi ambayo inachukua matrka mfumo wa kompyuta. Kulingana na chanzo hicho, faili zilinakiliwa kabla ya uwezekano wa kufichwa, na kuzifanya zisipatikane.
Katika taarifa yake, shirika hilo la ndee linarejelea “udukuzi haramu wa data nyeti,” bila kutaja maudhui yake. Data iliyoathiriwa inaweza kujumuisha taarifa za abiria, taarifa za wafanyakazi, na hati za ndani.
Shambulio hilo limedaiwa na kundi la INC Ransom, linalojulikana sana katika jumuiya ya usalama wa mtandao. Kundi hili linafanya kile ambacho wataalamu hukiita “ulafi maradufu.” Hasa, “wadukuzi huingia kwenye mifumo, hunakili data, na kisha wanazificha. Kisha wanatishia kuzichapisha ikiwa fidia haitalipwa,” anaelezea Dkt. Moussa Traoré, mtaalamu wa usalama wa mtandao.
Air Côte d’Ivoire inasema kwamba inashirikiana na mamlaka husika kutathmini kiwango cha tukio hilo, kupunguza athari zake, na kuimarisha ulinzi wa mazingira yake ya TEHAMA. Shirika hili la ndege pia linawahakikishia abiria kwamba ratiba yake ya safari za ndege itaendelea kama kawaida.