Sao Paulo, Brazil. Staa wa kimataifa wa Brazil, Neymar amesema kuwa anafikiria kustaafu kucheza soka katika miezi michache ijayo.

Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa akipata matatizo ya majeraha katika miaka ya hivi karibuni na amekiri kuwa kwa sasa haoni kama ataendelea kucheza kwa muda mrefu.

Neymar mwenye umri wa miaka 34 ambaye amewahi kupita Barcelona na Paris Saint-Germain, kwa sasa anaichezea klabu yake ya utotoni, Santos, baada ya kutoka kupitia kipindi kigumu cha majeraha ya mara kwa mara akiwa na Al Hilal ya Saudi Arabia.

Nyota wa zamani wa PSG ambaye kwa sasa anakipiga Santos, Neymar Jr. Picha na Mtandao

Hadi sasa, uhamisho wake wa usajili wa Pauni 200 milioni kutoka Barcelona kwenda PSG bado unashikilia rekodi ya ada kubwa zaidi ya usajili iliyowahi kulipwa kwa mchezaji.

Akizungumza na televisheni ya CazeTV kuhusu hatma yake na mipango yake ya baadae Neymar amesema: “Sijui nini kitakachotokea kuanzia sasa. Inawezekana Desemba ifike na nikataka kustaafu.”

Majeraha yamekuwa changamoto kwa Neymar tangu alipofikisha umri wa miaka thelathini, akiwa na vipindi virefu vya kukaa nje ya uwanja.

Mchezaji wa Santos, Neymar Jr ambaye aliwahi pia kuichezea Barcelona ya Hispania. Picha na Mtandao

Staa huyu anafahamu kuwa kurudi katika utimamu wake wa asilimia 100 kutahitajika endapo atataka kutimiza ndoto yake ya kuonekana katika Kombe la Dunia mwaka huu.

“Nimefanikiwa kurejea vizuri sana katika mchezo wa mwisho. Ninafurahi na nina utulivu kuwa nimeanza kurudi kidogo kidogo katika kiwango changu tofauti na ilivyokuwa kabla. Sijui nini kitakachotokea kuanzia sasa, itategemea na moyo wangu. Inawezekana nikaamua kustaafu kwa siku moja tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *